Fahamu Kuhusu Fantasy League Na Namna Ya Kushiriki #Fahamuzaidi

Maana;

Fantasy; Kitu cha kufikirika

Kwa hiyo unachokifanya hapa ni cha kufikirika!

Haya twende…

Fantasy Premier League inakuwaje?

Unapewa pesa kiasi cha paundi 100 ambazo utazitumia kununulia wachezaji 15 wanaocheza EPL.

Makipa wawili, beki watano, viungo watano, washambuliaji watatu.

Unachezaje????

Mfano wa Fantasy League katika picha.

 • Wachezaji wanakuwa na bei kulingana na performance zao

 • Bei ya juu kabisa ni paundi 13, ya chini kabisa ni paundi 4
 • Kwenye kila timu unaruhusiwa kuwa na wachezaji wa3 mwisho
 • Kila wiki unaruhusiwa kuuza na kununua mchezaji mmoja, ukizidisha unakatwa point 4 kwa kila mchezaji
 • Utapanga kikosi chako cha wachezaji 11 unavyopenda kila wiki
 • Wachezaji waliopo kwenye first 11 yako ndo watakupa points, waliopo bench hawatakupa unless kuwe na mchezaji hajacheza kabisa kwenye first eleven yako; hapo atafanyiwa sub automatic na ataingizwa aliyepo bench wa kwanza au aliyecheza; namna nyingine ya kupata point kwa wachezaji walipo bench imeelezewa chini

 • Wachezaji watapewa points kulingana na performance zao: mfano; goli: akifunga beki anapewa 6, akifunga kiungo anapewa 5, mshambuliaji anapewa 4. Akiassist anapewa 3, akiokoa penalty anapewa 5, akitoka na clean sheet anapata 6 (kipa na mabeki wake). Pia kuna bonus points kulingana na performance yake.
 • Kuna adhabu pia kama: akikosa penalty anakatwa point 2, akipata kadi, akijifunga n.k
 • Captain wa kikosi chako atapata points mara mbili: mfano akipata 10, mara 2 = 20
 • Kuna vitu vingine vingi, angalia kwenye picha au fungua link https://fantasy.premierleague.com/help/rules kisha ingia – Scoring

 • Kuna vitu pia vinaitwa chips: hivi vitu ni kama bonus kwa ajili ya kukusaidia; mfano wa chips 1) Bench boost – Kwenye hii chip points za wachezaji waliopo bench zitajumlishwa na utapewa, kuwa makini unapotumia chip hii maana inatumika mara moja kwa msimu mzima. Tumia chip hii pale unapokuwa na wachezaji wazuri bench na wenye uhakika wa namba. 2) Triple captain – Hii chip inakupa mara 3 ya points alizopata captain wako. Mfano akipata 10 zitazidishwa mara 3 = 30. Inatumika mara moja tu kwa msimu. 3) Wildcard – Hii chip inakupa nafasi ya kubadilisha kikosi chako chote bila kukatwa point yoyote ile. Inatumika mara mbili kwa msimu; mara moja mzunguko wa kwanza na mara moja mzunguko wa pili. 4) Free Hit – Hii chip inafanana na Wildcard; yaani unaweza kubadilisha kikosi chako bila kukatwa point; Isipokuwa tu, kikosi hicho kitatumika kwa wiki 1 moja pekee kisha kitarudi kile cha mwanzo. Inatumika mara moja kwa msimu.

Baada ya kutengeneza timu yako unaweza kujiunga kwenye ligi mbalimbali ambazo zinakuwa zimeanzishwa na watu. Unaweza kuunda pia ligi yako na ukawaunga washikaji.

Kama umeelewa tengeneza timu yako hapa https://users.premierleague.com/a/profile/register/personal

Tumia kifaa chochote, simu, laptop, desktop, tablet etc.

Pia unaweza kudownload app ya Premier League ambayo ndani ina Fantasy; Hakuna app official ya Fantasy Premier League.

Faida za FPL

Hasara za FPL

 • Inapoteza muda sana

Hizo ni dondoo chache kuhusu Fantasy Premier League, Una lolote tuachie hapo chini kwenye Box la Komenti pia unaweza kuongezea lolote unalojua kuhusu Fantasy Premier League.

Hits: 577