Jasho La Kwapani Kwa Mwanaume, Humsaidia Mwanamke Na Mzunguko Wa Hedhi #FahamuZaidi

Kama mwanamke atatumia jasho linalozalishwa katika kwapa kujipaka katika Lips za midomo yake basi itamsaidia sana katika kuamsha Hisia zao, na pia inasaidia katika kurekebisha mzunguko wa hedhi, hiyo ni kutokana na utafiti kama ulivyofanyika.

Unaambiwa wanaume wanatoa Kemikali zinazofahamika kwa jina la Pheromones ambazo zinatengenezwa katika nywele mbalimbali katika miili yao, ambazo kazi yake kubwa ni kumvutia Mwanamke, kama Mwanamke atatumia kujipaka katika Lips zake zitasaidia kuweka sawa mzunguko wa Hedhi.

Watafiti, walifanya kuwapaka wanawake Jasho kutoka kwenye kwapa wanawake 18 wenye umri wa miaka kuanzia 25 mpaka 45 ila hakuna aliyeambiwa kuwa alikuwa anapakwa Jasho la kwapa la Mwanaume.

Baada ya hapo waliulizwa kuangalia Hisia zao zikoje kwa masaa 6 baada ya kupakwa jasho hilo, ambapo wote walisema wanajisikia poa sana, zaidi hata ya mwanzo kabla ya kupakwa jasho hilo.

SOMA PIA: GAME OF THRONES NA WAIGIZAJI HALISI WA FILAMU ZA NGONO!

Charles   J. Wysocki, mtafiti kutoka chuo Kikuu cha Pennsylvania anasema ” Imetushangaza sana, Wanawake hao walisema kuwa walijisikia poa sana na katika msawazo mzuri zaidi hiyo ni baada ya kupakwa jasho hilo.”

Kemikali hizo zinazotolewa na Wanaume zinauwezo  mkubwa katika kubadirisha utendaji kazi kuanzia muonekano na kisaikolojia.

Kuhusu kurekebisha mzunguko fresh wa Hedhi, Kwa kawaida Homoni huwa zinakua kubwa sana na zenye haraka zaidi pale ambapo kitendo cha Ovulation kinapokuwa kinataka kufanyika.

Sasa Kemikali hiyo kutoka katika Jasho inasaidia katika kupunguza kasi za kuzalishwa kwa Homoni nyingine zaidi hivyo kuufanya mzunguko wa Hedhi kuwa poa zaidi.

Tuandikie, Nini unafikiri kuhusu utafiti huu?

Hits: 245