Faida Ya Supu ya Pweza #Fahamuzaidi

Kumekuwa na stori nyingi kuhusu uwezo wa samaki aina ya pweza pamoja na supu yake hususani wakiipa sifa nyingi katika utendaji wake mkubwa wa kuongeza nguvu za kiume.

Katika utafiti uliofanywa na Gazeti la Nipashe’ kwa kuwahoji wataalam mbalimbali wa Afya kutoka Hospitali mbalimbali pamoja na walaji uligundua faida kadhaa za samaki Pweza pamoja na supu yake.

Ulaji wa samaki Pweza katika mikoa ya pwani umeonesha kuwa na faida kubwa kwa walaji kimwili na kiuchumi kwa wauzaji

Kabla ya kwenda katika faida zake tambua samaki Pweza ana virutubisho kadhaa kama protini, mafuta (fats), vitamini B12, selenium, madini chuma (ron), shaba na pia vitamini B6.

Faida.

1. Husaidia katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume na mwanamke hii ni kutokana na uwingi wa Protini na madini ya Selenium kutoka kwa samaki Pweza ambayo huwa ni kichocheo kikubwa

2. Husaidia katika kuongezeka hali ya Uanamke’ na Uanaume’ kwa watumiaji. Katika mwili kuna vichocheo ambavyo hufanya kumtofautisha mtu katika Jinsia yake mfano Wanaume kuwa na sauti nzito. Pweza wana wana virutubisho vinavyochochea hali hiyo kwa jinsia zote mbili.

SOMA PIA: WANAUME WANA UWEZO WA KUBEBA MIMBA PIA

3. Faida nyingine husaidia kujikinga na maradhi ya kansa, tafiti kadhaa zinaonesha watu wanaokula sana pweza kuna uwezekano mdogo wa kupata kansa kama za midomo, matiti, shingo n.k

4. Faida nyingine huwasaidia kwaajili ya kuukinga ubongo kupungua uwezo wake wa kazi hii hususani kwa watu wenye umri mkubwa kitaalamu huitwa Alzheimer’

5. Husaidia pia kwa watu wenye matatizo ya pumu inaelezwa minofu ya Pweza ina virutubisho vinavyosaidia kupunguza athari za pumu.

6. Faida nyingine husaidia katika kusaidia kazi zingine za mwili kama mmeng’enyo wa chakula, upumuaji na mzunguko wa damu.

7. Kwa watu wenye matatizo ya kifua na upumuaji pia Pweza husaidia kupunguza athari hizo.

8. Faida zingine huongeza madini joto mwilini pia huongeza uzalishaji wa Haemoglobin ambazo ni muhimu katika damu.

Aidha inaelezwa pia ulaji sana wa Pweza huweza kusababisha Aleji hususani kwa watu wenye damu grupu 0′ lakini tafiti zingine zinaeleza kuwa wanawake wajawazito hawapaswi kutumia sana pweza sababu ya madini ya zebaki ambayo hupatikana mwilini mwake japo huwa kwa kiasi kidogo.

Una lolote la kutuambia kuhusu habari hii? Tuandikie katika boksi letu la Komenti pia usiache kutembelea mitandao yetu ya kijamii @fahamuzaidi FB, Twitter, Instagram na Snapchat.

Chanzo: Nipashe

Hits: 957