Stori Kuhusu Picha Ya Nyani’ na Hisia Kwa Mtoto Wake!

Wanyama huhisi maumivu kama namna Binadamu tunavyohisi hasa tunapopata taarifa za huzuni kama Kufiwa n.k

Nyani akionesha hisia kali baada ya kuhisi mtoto wake amekufa, picha ilipigwa kutoka nchini India’

Picha unayoona ilipigwa na Avinash Lodhi kutokea abalpur Madhya Pradesh, India ambae ni mwandishi wa habari za picha (Photojournalist).

Avinash anasimulia kuwa, ilikuwa ni jioni aliona kundi la nyani wakiwa wanacheza. Aliamua kuchukua picha kadhaa licha ya upungufu wa mwanga sababu ilikuwa ni jioni.

Mwandishi wa habari za picha Avinash Lodhi’ ambae alipiga picha ya nyani akionesha hisia kwa mtoto wake

Lakini ghafla mtoto wa nyani katikati ya michezo alionesha kuzimia na Mama (nyani) alionekana akionesha hisia kama kulia’ akidhani kampoteza mtoto wake.

Avinash anasema ” Hii picha ipo karibu sana na moyo wangu, niliipiga eneo la Jabalpur’ ilikuwa ni mwezi Aprili mwaka 2017, katika miaka yangu yote ya kupiga picha za wanyama sijawahi kupata picha yenye hisia kama hiyo”

SOMA PIA: MAISHA YA SIMBA DUME YANA MISUKO SUKO SANA.

Kitendo hicho kilitokea kwa haraka sana hata yeye mwenyewe anasema alikuja kugundua baada ya saa moja akiwa anazipitia picha hizo.

Kitu kizuri ni mtoto hakufa, ila namna Mama alivyoonesha hisia ya maumivu akidhani kampoteza mtoto wake inaonesha ni kwa namna gani wanyama nao huhisi maumivu pale wanapopoteza vitu wanavyopenda.

Kwa mujibu wa tafiti, Ukiachana na Binadamu Nyani ni mojawapo ya wanyama ambao hufanya msiba pale wanapoondokewa na mwanafamilia au jirani.

Una maoni yoyote? Tuandikie katika sanduku letu la maoni hapo chini usiache kutembelea #Fahamuzaidi katika mitandao yetu yote tunapatikana kwa jina la #Fahamuzaidi sehemu yoyote ambayo upo.

Hits: 980