Unataka Kupakua Filamu & Series? Fuata Hatua Hizi!

Watu wengi katika mitandao yetu wamekuwa wakiuliza namna ambavyo wanaweza kupata filamu katika Chaneli yetu ya telegram.

Haya ni maelezo yote namna ya kupata Filamu mbalimbali tunazoweka katika Chaneli yetu ya Telegram inayokwenda kwa jina la#FahamuMovies.

Jambo la kwanza.

Hakikisha simu yako ina uwezo mzuri wa katika matumizi ya intaneti na pia ina nafasi ya kutosha ili kuruhusu uwepo wa Application zingine.

Jambo la pili

Kama simu yako inatumia mfumo wa Android’ Bonyeza HAPA kupakua Application Ya Telegram, Kama simu yako inatumia mfumo wa iOS kwa maana ya watu wanaotumia iPhone bonyeza HAPA.

Jambo la tatu

Muonekano wa Chaneli ya #FahamuMovies katika Telegram

Ukishapakua kinachofuata ni kujiunga na chaneli yetu ambapo kama Bado Bonyeza HAPA lakini kama tayari upo katika Chaneli yetu basi Ondoa shaka.

Mambo muhimu.

Hakikisha unatumia Player hii, Kama unatumia simu ya Android au iphone pakua Player ya VLC PLAYER ambayo ni muhimu kwa sababu ina uwezo wa kufungua Fomati zozote zile bila tatizo. Lakini kwa watu wa Android’ unaweza kupakua hata Player inaitwa MX PLAYER.

Bonyeza HAPA kwa mtu wa Android kupakua VLC kama bado, Na mtu wa iphone Bonyeza HAPA kushusha sasa.

Kuna matatizo kadhaa yanawapata watu mfano, Unabonyeza Filamu lakini inakuwa inazunguka Tu bila kupakua, Kama unapata tatizo hilo tumia Telegram X.

SOMA PIA: FANYA HIVI KUPATA SUBTITLE YA FILAMU AU SERIES YOYOTE ILE.

Telegram ya kawaida kwa watu wengi imekuwa ikiwasumbua hususani katika matumizi hivyo nakushauri utumie Telegram X.

Watu wa iphone kuna muda unaweza ku Play filamu alafu ikakupa ujumbe kama huu 👇

Fanya hivi bofya alama upande wa kulia ambayo imeonesha kamshale kajuu.

Bonyeza katika eneo ambalo limezungushiwa na alama nyekundu

Kisha bonyeza hapo Copy to Vlc” utaona itaanza kuonesha.

Ukifika hapa, Bofya Copy to Vlc’

Unapata vipi kitu ulichopakua katika Telegram?

Folda la Telegram’ linapatikana katika Memory Card yako lakini huwa linajificha.

Hivyo cha kufanya ni kutafuta sehemu ambayo unaweza Ku search’ na andika Telegram’ utaliona au ukitumia waya wa Usb katika Kompyuta yako kulitafuta katika simu yako pia utaliona ambapo vitu vyote unavyopakua vinakuwepo huko.

Baada ya kutafuta katika Memory Card yako.

Lakini kuna baadhi ya vitu kama Picha na video’ unaweza usizikute katika Memory yako kwani ni lazima ufanye saving ili uvipate katika Memory card yako.

Unataka kuzifuta Filamu & Series?

Nenda katika setting kama unavyoona 👇

Baada ya hapo bonyeza Data and Storage 👇

Bonyeza tena Storage usage

Maliza sasa unachotaka kukifuta 👇

Umefuata taratibu zote hizi na bado unaona kuna tatizo, basi tuandikie Kupitia Instagram yetu ya FahamuMovies katika DM yetu au barua pepe habari@fahamuzaidi.com

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 3122

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!