Maisha Ya Simba Dume Yana Misuko Suko Ya Kutisha

Simba ni mnyama anayesifika kwa ukali mpaka kubatizwa jina la mfalme wa nyika.

Cheo cha ufalme wa nyika hauendi kwa simba jike bali cheo hicho ni mahususi kwaajili ya simba dume.

Wapo wanaodhani simba dume ni mzembe sababu mara nyingi hashiriki kwenye kuwinda na kuleta kitoweo bali simba jike ndiye anaye hustle sana kuwinda na kuua kitoweo,wengi wanaowaza hivi hawaelewi vizuri majukumu na kazi ya simba dume.

Simba hupendelea kuishi kwa mtindo wa familia pale simba wanapozaa watoto hutambulika kwa jina la pride tuseme kwenye familia kuna simba dume ,jike na wadogo zake sasa huyu jike akipewa mimba na akizaa sasa rasmi kikundi hicho cha simba hujulikana kama pride.

SOMA PIA: KIASI CHA PESA GOOGLE WANALIPA KWA APPLE INASHANGAZA!

Kwa kuwa makala yetu imejikita kuzungumzia maisha ya simba dume basi tujikite kwenye mada husika ,mara nyingi simba akijifungua jike wanakuwa wengi na dume wachache.

Hawa watoto watalelewa vizuri kwa kupatiwa maziwa mpaka pale watakapofikia hatua ya kula nyama.

Maisha ya watoto hawa wote jike na dume huwa ni ya furaha wanacheza ,wanakula na kufanya kila kitu na hata kuchezea sharubu za baba.

Maisha huanza kubadilika baada ya watoto hawa kufikisha miaka 2 kamili au kasoro ,jike wataishi kama awali kula ,kucheza ,kufanya utundu nk lakini simba dume akifikisha umri huo huwa anakuwa makini sana hata fujo ,utundu huwa hafanyi na pindi mnyama akiuliwa kwaajili ya kitoweo simba huyu huwa hagombanii chakula.

Endapo baba yake akitaka kipande kikubwa cha nyama na kuleta ubabe mtoto huyu wa kiume hujisogeza pembeni ila watoto wa kike wanaweza kudinda.

Maisha ya mtoto wa kiume akishafikisha umri huo huwa hamjaribu kabisa baba yake na pia mzee simba huwa anamvutia sekunde ,dakika ,saa ,siku ili amvae mwanaye na amchane ukweli.Endapo mtoto huyu wa kiume aki test uvumilivu wa mzee kwa kugombania msosi ,kufanya mautundu ,kucheza na shangazi zake basi mzee simba uvumilivu utamshinda.

Simba dume akishafikisha miaka 2 huwa anasubiria sekunde ,saa au siku atimuliwe na baba yake kwenye familia aende kujitegemea huku watoto wa kike wakibaki kwenye familia kupata msosi wa bure.

SOMA PIA: GAME OF THRONES NA WAIGIZAJI HALISI WA FILAMU ZA NGONO!

Siku mzee simba frustrations zikimjaa humvaa mwanaye wa kiume na kumfukuza kwenye eneo lake na simba dume huwa ana miliki eneo mpaka mile 10,na simba kijana lazima asepe na hapa mzee simba huwa ni mkali hana msalia mtume anamfukuza kwa ukali kama vile hamjui mwanaye kama vile sio damu yake hapa simba kijana husepa zake na mzee simba humfukuza huyu kijana mpaka ahakikishe kashaondoka katika eneo lake la mile 2,3 ,10 nk .

Hapa simba huyu kijana mwenye miaka 2 au 2 kasoro akiwa ndio anaingia kwenye balehe ila bado hayupo fiti anajisepea zake huku akitizama nyuma haamini anaachana na mama yake ,ndugu zake.simba huyu huanza maisha mapya akiwa pekee yake.

Simba huyu atakutana na vikwazo vingi njiani kwanza fisi ,inatambulika fisi na simba ni maadui na fisi huishi kwa ukoo..koo moja ya fisi inaweza kufikisha idadi ya fisi 18 .

Sasa simba huyu kijana akikutana na fisi hawa ataweza kushambuliwa tu na meno ya fisi ni makali kuliko mnyama yeyote yule sasa simba huyu akiwekwa kati na fisi wakamzunguka kama akinusurika basi ni majeraha na simba akipata majeraha ina maana atashindwa kuwinda na kifo kitamsogelea.

Pili simba huyu ataingia eneo la simba dume na hakuna jambo hatarishi kama kupita au kuingia eneo la simba dume hapo lazima kiwake na kwakuwa simba huyu aliyefukuzwa kwao bado mdogo lazima ataumizwa vibaya kama sio kuuliwa.

SOMA PIA:THE GREAT WALL UJENZI WA BINADAMU ULIO MREFU ZAIDI!

Kwenye suala la uwindaji simba hupenda kuwinda nyati kwakuwa nyati hana spidi sana na ni kitoeo kikubwa na nyati mmoja hukalishwa chini na simba 4,5…sasa simba huyu anayeanza kubalehe ataweza kumkalisha nyati ? La hasha

Simba hawindi swala ni aghalabu sana simba kuwinda swala sababu swala ana mbio sana na simba hana mbio za kumkimbiza swala huwa inatokea simba anavizia kwa kunyata mpaka ahakikishe amefika mita 3 au 2 ndio amstukize swala..chakula kingine cha simba ni nyumbu na pundamilia

Kwakuwa simba huyu alikuwa anashiriki na mama ,shangazi ,Dada zake kwenye kuwinda basi instincts za kuwinda anazijua ila simba huwa wanapenda kuwinda kwa ushirikiano na yeye yupo pekee yake hapa ndio shida ilipo.

Kama simba dume walizaliwa 2 basi hufukuzwa pamoja na simba ndugu huwa wanapendana sana hivyo inakuwa bahati simba hawa watashirikiana kwa kila kitu kwenye kuwinda ,kupigana na adui nk na kama yupo pekee yake basi ataishi maisha yake kwa uangalifu na ugumu kiasi labda itokee akutane na simba dume mwingine aliyefukuzwa na mzee wake na wataunda timu moja na sababu kubwa ni kwaajili ya kuwinda ,ushirikiano wao utakuwa umekutanishwa na lengo moja kuwinda na watakaa pamoja kwa muda kidogo na baada ya muda kila mmoja atachukua hamsini zake.

Maisha yataenda hivyo mpaka atakapofikisha miaka 5 hapo atakuwa shababi haswa na atakuwa na misuli mikubwa na nywele nyingi hata ukimuona lazima utetemeke ,akikutana na koo ya fisi wapatao 15 lazima fisi hao watimue mbio wote ,mngurumo wake husikika kwa umbali wa mile kadhaa.

SOMA PIA: KICHECHE MNYAMA ASIYEWEZA KUISHI BILA KUJAMIIANA!

Kwa umri huu aliofikisha simba huyu anakuwa kivuruge chochote humwambii yupo kwenye peak yake ,akimuona simba jike pekee yake ataenda kumtongoza na simba jike huyo hatomkubalia kirahisi kwanza atampima ubavu je yupo fiti ,je ataweza kumlinda yeye na watoto ,akisha thibitisha hilo ndio ataruhusu kuwa nae na hapo watafanya mapenzi sana hata mara 35 kwa siku .

Simba huyu asipopata jike maana ni aghalabu sana kumuona simba jike awe pekee yake basi atatakiwa aingie kwenye eneo linalomilikiwa na simba na hapo watapigana na akishinda atalimiliki hilo eneo na jike waliokuwepo na kama jike atakuwa na watoto basi atawaua wale watoto wake ili aweke damu yake na genes zake na endapo akipigwa basi atapigika kiukweli na kuumizwa vibaya na kutimuliwa.

Endapo akishinda pambano simba anayemiliki eneo ataondoka na simba huyu atajitawalia eneo hilo na ataweka alama ili simba yeyote mvamizi akitokea apate onyo hii sehemu ni hatari hupaswi kuwepo.,endapo wakizaa watoto na jike basi wataitwa pride na simba jike huwa wanaenda kuwinda huku dume akiondoka zake kwenda kutizama mipaka na hutembea mile kuhakikisha hakuna mvamizi yeyote anaingia kwenye ardhi yake kisha ana nguruma na mngurumo huo husikika kwa umbali wa mile kadhaa kama kutoa tahadhari kwa madume wengine kuwa eneo fulani kuna mfalme hivyo haipaswi kuingia na kama kuna dume karibu haswa wadogo au wasio tayari kupambana basi huondoka zao ,simba dume huyu akishafanya patrol ya eneo lake huweka alama ili hata dume yeyote akikatiza kwa bahati mbaya apate tahadhari na onyo hilo kisha hurudi kwa familia yake na jike wakishawinda wa kwanza kula ni dume na ukiwa mbishi utakutana na kisago sababu huyu dume hufanya kazi kubwa hivyo lazima ale ashibe

Simba dume maisha yake yote hutegemea nguvu ,ndio maana kila siku anakagua eneo lake na kutoa tahadhari kwa simba wengine lakini lazima akumbane na misukosuko wapo simba dume ni mabachelor nao wanataka familia na msosi wa bure na njia rahisi ni kuvamia eneo la pride na kupigana na dume mpaka kieleweke ,simba hutofautiana wapo wanaotembea kindugu wawili wawili haswa waliozaliwa tumbo moja hawa wanapovamia eneo linalomilikiwa na simba mmoja ni rahisi wao kushinda na eneo linalomilikiwa na simba dume 2 ni vigumu kupokwa na wavamizi.

Siku zote mapambano ya simba dume kugombea na kulinda eneo huleta maafa makubwa;

1.simba wanapopigana hukimbilia kung’ata na kunyofoa mapumbu na simba aliyenyofolewa mapumbu hushindwa tena kuzalisha na kusambaza damu yake ,

2.simba anayeshindwa huwa anaumizwa vibaya sana mithili ya mtu aliyegongwa na fuso na wengi hufa sababu simba ni mbishi,hakati tamaa kwenye kupigana

SOMA PIA: SIO WANAWAKE TU HATA WANAUME HUPATWA NA HEDHI!

3.endapo simba mvamizi akishinda pambano basi vitoto vyote huuliwa labda mama simba akiona mumewe kazidiwa hukimbia na watoto na kuwaacha majike wengine ambao watatawaliwa na simba mpya huyo

Haya ndio maisha ya simba dume hakuitwa mfalme wa nyika kwa bahati mbaya ,simba humiliki mile kadhaa za eneo wanyama wote nyati,nyumbu,pundamilia,twiga na hata tembo ni wa kwake sasa ole wake simba mwingine au fisi ajipendekeze kwenda kuwinda eneo lake atauliwa kama sio kujeruhiwa.

Simba maisha yake mengi hutawaliwa na hofu ya kupinduliwa ndio maana mwanaye wa kiume akifikisha miaka 2 humfukuza ,jihadhari sana kuingia kwenye territory ya simba hautobaki salama bora ukutane na jike kuliko dume utararuriwa tu.

Imeandikwa na Junky

Hits: 425