Prahlad Jani Mzee Aliyeishi Zaidi Ya Miaka 75 Bila Kula Wa Kunywa Chochote!

Kuna mambo kama ukiambiwa unaweza usiamini kwa sababu unajua pengine ni tofauti kabisa na namna unavyofahamu wewe.

Tuliandika kwa dondoo katika mitandao yetu ya kijamii kuhusu mzee huyu ambae yeye mwenyewe alisema kuwa ana zaidi ya miaka 75 hajawahi kula wala kunywa chochote.

SOMA PIA: JONAS SALK, MGUNDUZI WA CHANJO YA POLIO ALIGOMA KUIWEKEA HATIMILIKI YAKE!

Pengine ni jambo kubwa sana la kushangaza, inakuaje mtu hajala wala kunywa kwa miaka yote hiyo wakati inafahamika kuwa kwa binadamu wa kawaida kama utakosa chakula na maji, basi ndani ya siku tatu hali kwako itakua tatizo.

Mzee Prahlad Jani amezaliwa mwaka 1929 na anasema hajawahi kugusa kitu chochote tangu mwaka 1940.

Inakuaje mpaka sasa Yupo hai?

Kwa maelezo yake mwenyewe anasema kuwa anapata nguvu kutoka kwa mungu wake anaefahamika kwa jina la Amba ambae ndiye aliyempa muujiza huo ambapo pale anapokuwa anasikia njaa kuna kama shimo katika mdomo wake juu karibu na matundu ya pua, ambalo humpa kitu kama mate mate yanayomfanya asisikie kutumia kitu chochote kile pale anaposikia kama njaa.

Mwaka 2003 alifanyiwa vipimo na utafiti na madaktari ili kugundua ukweli wa jambo hilo ambapo majibu waliyopata.

Kwanza alifanyiwa majaribio kwa siku 10, madaktari wanasema kuwa hawakuwahi kumuona akipata chakula au maji na uchunguzi wa mwili wake ulipofanyika Mwili ulionesha kuwa poa.

SOMA PIA: FAHAMU NAMNA YA KUPATA SUBTITLE YA FILAMU AU SERIES YOYOTE!

Mkojo ulioneshwa kutengenezwa katika kibofu lakini ulikuwa ukifyonza na mwili wake jambo ambalo walikuta sio la kawaida na kingine walichoona zaidi ni tundu dogo ndani ya mdomo juu kidogo ya matundu ya pua.

Mwaka 2010 utafiti mwingine tena ulifanyika na majibu waliyopata yalikua ni hayo hayo, mzee hawakuwahi kumuona kwenda chooni au kula chochote.Huyo ndio Prahlad Jani.

Vyanzo: Wikipedia, Lightdocumentary.com, Wikiversity.org.

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 246

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!