Kiasi Cha Pesa Google Wanalipa Kwa Apple, Inashangaza!

Kuna kitu cha kujifunza hapa, ushawahi kujiuliza kwanini makampuni makubwa licha ya kufahamika na watu kila siku yamekuwa yakizidi kuchangamkia fursa mbalimbali za matangazo.

Kuna siri kubwa juu ya nguvu ya matangazo, Licha ya Google kuwa moja ya Search Engine’ ambazo zinatumiwa kwa kiasi kikubwa na watu katika vifaa vya mawasiliano lakini hiyo haiwafanyi kuacha kuhakikisha kila siku wanaendelea kuwa juu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Business Insider mwaka 2018 Google pamoja na Apple waliingia katika makubaliano mapya ambapo Google’ walilipa Tsh Trilioni 20 na mwaka 2019 imeripotiwa kuwa wamelipa Tsh Trilioni 27.

Muonekano wa Google katika kivinjari cha Safari’

Uwepo wa Google kwenye vifaa vya Apple kama iPhone, Mac na iPad imeonekana kuwa na faida kubwa kwa Google hasa kutokana na ubora wa vifaa na watumiaji wake wengi ambao hupenda kununua vitu mtandaoni.

Hivyo hiyo imekuwa ni sababu kubwa sana kwanini Google wanatoa kiasi kikubwa cha pesa, sababu ikiwa ni kuendelea kutengeneza faida sababu wateja wake kwa kiasi kikubwa pia wanapatikana katika bidhaa za Apple!

Kuna uwezekano mkubwa wa dili la Apple na Google likazidi kukua kila siku hasa kutokana na pesa ambayo Google wamekuwa wakilipa imeonekana ikizidi kuongezeka kwa kila mwaka.

Una lolote kuhusu habari hii, tuandike hapo chini katika sanduku letu la maoni. Kama bado pita chini kabisa kujiunga katika mitandao yetu ya kijamii ili usipitwe na habari mbalimbali.

Hits: 516