Avengers:Endgame Ujio Mpya Ubora Ule Ule, Je Kipi Kinafuata!

Avengers: Endgame imeachiwa rasmi Aprili 26 katika kumbi za kuonesha filamu sehemu mbalimbali duniani.

Tangu imeachiwa imepewa sifa kubwa sana, wachambuzi wa masuala ya filamu wametoa sifa hasa katika upande wa uigizaji pia na hisia namna ilivyojengwa.

Binafsi nimependa pia waigizaji kwa kila mmoja wamefanya jambo kubwa kwa kutimiza wajibu wao lakini nimependa mpangilio wa uandishi wa Scenes…upande wa uandishi ni hakika nakiri binafsi hakuna matata.

SOMA PIA: NAMNA YA KUPATA SUBTITLE YA FILAMU YOYOTE KWA HARAKA ZAIDI

Kama kawaida nilitegemea kuona vichekesho vya hapa na pale lakini kitu poa zaidi ilikuwa ni muonekano mwingine ya waigizaji wote ambao walipotea katika Infinity War.

Kuhusu Endgame kama hujatazama filamu za nyuma kama Iron Man 2, Thor, Hulk n.k ambazo zimetoa mtiririko wa stori ambayo imekuja kuhitimishwa kwenye Endgame basi hii filamu utaiona ni mbaya.

Wakati natazama nilikuwa naangalia kujaribu kuona utofauti wowote au kitu kipya zaidi cha utofauti lakini binafsi sijaona zaidi ya Ubora ule ule kuzingatiwa kwa kiasi kizuri zaidi.

Thanos’ katika Avengers: Endgame Jitu lenye unyama wake 😉

Haichoshi kuitizama hasa kutokana na mpangilio wake pamoja na utani kadhaa wa hapa na pale wa wahusika unakufanya uendelee kusubiri kuona mwisho wa Thanos” namna ipi watavyommaliza.

Muonekano ni bora utumiaji wa Effects hapa sikuwa na shida sababu Marvel wanajua wanachokifanya. Wengi tulitegemea kuona Captain Marvel ndiye atakae maliza kila kitu lakini Iron Man kama tulivyoona ndiye aliyemaliza mchezo mzima.

Na pia tumeona mwisho wa Black Widow’ na Iron Man’.

Tony Stark na Scarlet katika Iron Man 2 😊 unakumbuka?

Hawa ni wahusika ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa na uhusiano wa ukaribu… binafsi, sijajua nini kitaendelea baada ya kifo cha Iron Manambae ndiye alikuwa kila kitu katika kuratibu mipango yote ya kiteknolojia lakini hata ki pesa.

Nini kinafuata?

Baada ya End game, Marvel wana mpango wa kuachia filamu tatu tatu kwa kila mwaka kuanzia mwaka 2020 mpaka 2022. Bado haijafahamika zitakuwa ni filamu za aina gani lakini wataalamu wengi wa masuala ya filamu wana imani kuwa itakua ni mwanzo mpya wa kuja kivingine katika kutengeneza Avengers nyingine mpya.

SOMA PIA: KICHECHE MNYAMA ASIYEWEZA KUISHI BILA KUJAMIIANA

Tusisahau kuwa Spider-Man: Far From Home inakuja July 2 mwaka huu, na Tom Holland kutoka mkataba wake alisaini filamu 3 za Spider-Man hivyo kuna moja bado inabaki.

Spider-Man : Far From Home inaachiwa rasmi sehemu nyingi duniani July 02, hii itakuwa filamu ya pili kumuona Tom Holland akicheza kama Spider-Man

Tunategemea ujio kadhaa wa Filamu za kipekee kama Black Widownafasi iliyochezwa vyema na Scarlet Johansson’ Marvel wametangaza mara kadhaa wana mpango wa kuja na filamu ya pekee (Solo)

Black Widow’ Scarlet Johansson katika moja ya filamu za Avengers

Filamu zingine ambazo zinatarajiwa kurudi tena ni

Black Panther baada ya kufanya vizuri katika sehemu ya kwanza inatazamiwa kurudi hivi karibuni na tayari mipango kadhaa imeanza kufanyika

Black Panther 2, Guardians of the Galaxy vol 3, Doctor strange 2 na zingine ambazo zinatazamiwa kwa jicho la mbali mbali ni Hawkeye‘ pamoja na Wanda vision’

Bado hujatazama Avengers: Endgame unaweza pita Hapa ujipatie pia kazi kadhaa zingine kutoka mtiririko mzima kabla ya The Avengers: Endgame.

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 1234

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!