Mwanaume Una Uwezo Wa Kubeba Mimba’ #Fahamuzaidi

Kuna mambo ukiambiwa kuamini huwa ni utata hasa kutokana na mantiki ambayo imejengeka na kufahamika tangu muda.

Inafahamika kuwa wanawake ndiyo wenye uwezo wa kushika mimba na kuzaa na wanaume ndiyo wenye uwezo wa kutoa mbegu kwaajili ya kusababisha mimba.

Kwa lugha rahisi, Mwanamke hawezi kujipa mimba mwenyewe na mwanaume hawezi kubeba mimba, Lakini kwa mujibu ya Wanasayansi unaambiwa kwa mwanaume kushika mimba na kuzaa inawezekana.

Kivipi?

Kushika mimba na kuzaa kwa mwanaume inawezekana lakini kwa kufuata taratibu maalumu. Hapa nitaelezea taratibu mbili ambazo zimeonesha kuwa ndizo zinawezekana na kutoa mafanikio makubwa.

1. Kwa wanaume ambao walizaliwa wakiwa na Homoni nyingi za kike kuliko za kiume

Kwa mujibu wa Tovuti ya Heathline inaeleza kuwa, sio kila mwanaume huwa ni mwanaume. Kuna wengi tangu akiwa mtoto alizaliwa akiwa na sifa kwa maana ya taratibu za Homoni nyingi za kike kuliko za kiume. Kwa mtu kama huyu kumpandikiza Mimba inawezekana kwa sababu kuna vitu halisia vya kusapoti mimba.

2. Wanaume waliobadilisha jinsia, nao hawa pia wanaweza kupata mimba na kuzaa vizuri tu. Lakini hapa itategemeana na namna ya upasuaji wake wa kupandikiza jinsia ya kike ulivyofanyika ambapo kitendo hicho kinahitaji umakini mkubwa sana.

Kuzaa

Ni lazima iwe kwa upasuaji sababu kwa njia ya kawaida hata kama mwanaume atakuwa kawekewa jinsia ya kike kuzaa kwa kutumia njia hiyo huwa ni hatari. Hivyo njia kuu huwa ni upasuaji ambayo ni salama zaidi.

Njia kuu ni upandikizaji.

Njia pekee ambayo mwanaume anaweza kubeba mimba ni kwa upandikizaji na si vinginevyo japo kwa wanaume waliopandikizwa njia ya uzazi inawezekana kupata mimba kwa njia ya kawaida kwa maana ya kujamiiana.

SOMA ZAIDI HAPA!

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 598

2 thoughts on “Mwanaume Una Uwezo Wa Kubeba Mimba’ #Fahamuzaidi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!