Sio Wanawake Tu, Hata Wanaume Pia Hupatwa Na Hedhi!

Hii inaweza kuwa ngumu kumeza kwa watu wengi hususani kwa wanaume wenyewe kuamini kuwa hupatwa na hedhi.

Kwa mujibu ya wanasayansi wamebaini kuwa Wanaume nao hupatwa na hedhi lakini ni kwa utofauti sio sawa kama inavyowatokea Wanawake.

Kisayansi ni Ndio lakini kwa Wanaume ni tofauti sana, sio kama Wanawake ambao Yai (Ovum) likipasuka basi ute uliochanganyikana na damu huanza kutoka, na pengine hilo ndilo linasababisha inakua kazi kumgundua mwanaume nae pale anapokua katika siku zake (Hedhi).

Kulingana na tafiti zimebainisha kuwa, Wanaume pia huenda mfumo wa mzunguko na mabadiriko ya Homoni zao kama wanawake ambavyo hutokea katika siku zao (Hedhi) kwa kila mwezi.

SOMA PIA: ZIWA KISIBA NA SIMULIZI YA NYOKA YENYE VICHWA VIWILI!

Mabadiriko ya homoni hayo kwa Wanaume huitwa “Irritable Male Syndrome” (IMS) lakini kwa wanawake huitwa Premestrual Syndrome (PMS)

Kutokana na hilo, husababisha Homoni ya “Testosterone” kupanda na kushuka mara kwa mara kwa siku na wakati mwingine mpaka kwa mwezi lakini Wanasayansi wanasema pia asilimia kubwa huchagizwa na mazingira ya mtu tofauti na wanawake ambao wao ni yai likishindwa kurutubishwa.

SOMA PIA: FAIDA YA SUPU YA PWEZA

Kutokana na kupanda na kushuka kwa kiwango cha Testosterone utaweza kumgundua Mwanaume huyo kwa tabia kadhaa kama mtu kuwa na Hasira, huzuni, Ukali kupindua na tabia zingine za tofauti na hali ya mtu kama unavyomjua.

Kikawaida kumgundua Mwanaume kama tulivyosema mwanzo ni kazi, lakini kama atapimwa kiwango chake cha Testestorone basi anaweza kugundulika kama yupo katika siku zake ama Laah…

Hitimisho: Katika kutokea kwa Hedhi kwa Mwanamke, Ni tendo la kufeli pia kwa Homoni au kushuka kwa Homoni ya Progesterone hasa baaada ya Yai kukosa mbegu ya kurutubisha, hivyo kutokana na kushuka huko pamoja na Estrogen ndiko husababisha Yai kupasuka na kuanza Kutoka.

Hivyo kwa wanaume, nao kumbuka wana Estrogen, lakini mratibu mkuu ni Testestorone ambapo zikipanda na baadae zikishuka sana ndipo hali ya siku zake hutokea.

Kwa maswali, maoni au Kuongezea tuachie katika Box letu la maoni.

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 1348

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!