Fahamu Namna Ya Kupata Subtitle Ya Filamu/Series Yoyote Unayohitaji Kwa Haraka!

Kutazama filamu ambayo ina Subtitle kuna raha yake hususani katika kuelewa kwa ufasaha kinachoendelea katika filamu au series fulani.

Hapa nitaenda kukuonesha ni njia ipi ambayo utaweza kupata Subtitle ya filamu au Series yoyote unayohitaji. Kabla hatujaenda mbali zaidi, Zoezi hili linaweza kufanikiwa kama unatumia Kompyuta au Simu ambayo inaruhusu intaneti vizuri.

Hapa nitakuonesha tovuti kadhaa bora zaidi ambazo zitakupatia Subtittle yoyote unayohitaji kutokana na hitaji lako husika.

1. Subscene

Tovuti hii ya Subscene itakupatia machaguo mbalimbali kwa uharaka zaidi na usahihi

Hii ni tovuti ninayoipenda kuitumia kila mara pale ninapohitaji Subtittle yoyote na sababu kuu za kuipenda ni namna ambavyo kila siku vitu vipya huongezwa na yote ni kwa sababu wanaoiendesha kwa kiasi kikubwa ni watumiaji wenyewe kama mimi na wewe ambao wamepewa nafasi ya kuweza ku Upload…Hivyo hata wewe ukihitaji kuweza kuwasaidia wengine kupata Subtitle unaweza kuwa na akaunti na ukawa una Upload pia.

SOMA PIA: KICHECHE MNYAMA ASIYEWEZA KUISHI BILA KUJAMIIANA

Fomati ya Subtitle nyingi zipo katika mfumo wa SRT ambao ni mzuri katika mafaili ya subtitles mbalimbali.

Kingine ninachopenda ni uharaka wakati unapotafuta unachotaka lakini zaidi ni uwepo wa Data nyingi zaidi ya subtittle mbalimbali.

2. Subtitleseeker

Muonekano wa subtitleseeker tovuti nyingine bora katika utafutaji wa Subtittles mbalimbali

Hii tovuti ambayo kazi kubwa inayofanya ni kukupa vyanzo mbalimbali ambavyo utapata Subtittle kwa haraka zaidi. Uzuri wa hii ni uharaka wake pale ambapo unapokuwa unatafuta Subtittle fulani na ni nadra kukosa hitaji lako.

Kitu kizuri zaidi kuhusu hii Tovuti ni namna inavyotoa vipengele mbalimbali kama vya Filamu mpya ambazo tayari unaweza kupata Subtittle mbalimbali na mjumuiko wa masuala mengine pia.

3. Open Subtittle

Opensubtitle ni maarufu kwa watumiaji wengi pengine ni kutokana na uwezo wake wa kutoa majibu fasaha katika uhitaji wa filamu mbalimbali

Hii inatumiwa sana na watu wengi, pengine ni kutokana na uharaka wake ni urahisi pia. katika tovuti hii hakuna mambo mengi ambayo yanahitajika zaidi ya kutafuta hitaji lako na kwa uharaka unaweza kupata kisha kuweza kutumia.

Uzuri wa hii pia ni uwingi wa taarifa za Subtittle pengine ndiyo maana inapendwa zaidi. Kuna tovuti nyingi ila kwa ubora zaidi nimetaja Hizo tovuti tatu sababu zipo vizuri sana katika kuhakikisha unapata jibu halisi kwa kile unachotaka.

Namna ya kuziweka

VLC Player ni rahisi zaidi katika uwekaji wa Subtitles mbalimbali kwa njia rahisi na haraka

Hapa utahitaji uwe na Player ya VLC ambayo hutoa uwezo wa kuweza kuongeza Subtitle ambayo umepakua.

Cha kufanya ili uweze kutazama filamu pamoja na Subtitle ulizopakua cha kufanya fungua Filamu katika player ya VLC kisha nenda sehemu ya Option utaona sehemu imekuandikia Subtittle au Add Subtittle ukibonyeza hapo itakuonesha kuhitaji Faili ambalo umepakua ili uweze kuweka sasa.

SOMA PIA: THE GREAT WALL: UJENZI WA BINADAMU MREFU ZAIDI

Ukichagua faili hilo la subtitle ambayo ulipakua na kuweka hapo basi Automatic utaanza kuona maandishi chini ya hitaji lako yametimia.

Hakuna ugumu wowote, Cha msingi kuwa makini unapopakua hilo Faili la Subtitle liweke sehemu ambayo itakuwa rahisi kulipata mfano katika Desktop yako ili lisikusumbue utapokuwa unahitaji kulitumia.

Una swali lolote au kuongezea tuandikie hapo chini katika kiboksi chetu cha maoni!

Mhariri

Kazi yangu ni kukufahamisha zaidi yale usiyoyajua. Kumbuka Elimu haina mwisho.

More Posts

Hits: 5516

9 thoughts on “Fahamu Namna Ya Kupata Subtitle Ya Filamu/Series Yoyote Unayohitaji Kwa Haraka!

  1. Nimejaribu sana kupata subtitle za Vis a vis (locked up) from season 2 bila mafanikio evn hzo umeonesha nimekosa 😭😭

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!