The Great Wall: Ujenzi Wa Binadamu Ulio Mrefu Zaidi!

Ulianza kujengwa miaka 2,000 iliyopita mpaka sasa unaurefu wa kilometa zaidi ya elfu sita (6000km) na ndio ujenzi pekee wa binadamu ulio mrefu zaidi duniani kote kwa utambarare sio kwenda juu.

Muonekano katika ramani ukuta wa China (The Great Wall)

Wachina walijenga kwaajiri ya usalama wao hasa kujikinga na maadui kutoka upande wa kaskazini.

Ukuta huu unaupana wa mita tisa tu (30ft) ambayo ni sehemu nzuri ya kutembea kwa miguu na kunamaeneo mengine ni salama hata kuendesha magari.

Muonekano wa ukuta wa China

Ukuta huu ulijengwa na watumwa na wanajeshi kwa awamu mbalimbali na zaidi ya watu milioni moja warifariki katika ujenzi huo. Zaidi ya watu milioni 10 hutembelea eneo hilo maarufu kwa utalii. Ukuta huu unapatikana katika mji mkuu wa china.

Toroli (Wheel barrow) liligunduliwa na wachina katika ujenzi wa ukuta huu.

Katika hatua za mwanzo, Unga wa mchele ulitumika kuunganisha matofali (Kama gundi) wakati wa ujenzi.

Jina la China lilitokana na sehemu ndogo ya ukuta huo iliyokuwa ikiitwa “Qin Shi Huang” ambapo “Qin” inatamkwa “Chin”.

Una lolote la kuongezea kuhusu Ukuta wa China (The Great Wall) tuandikie kupitia sanduku letu la maoni hapo chini.

Picha kwa msaada wa mtandao.

Hits: 389