Kicheche: Mnyama Asiyeweza Kuishi Bila Kujamiiana!

Kicheche’ ni mnyama mdogo ambae anapatikana sana katika ukanda wa Savana, kwa kifupi maeneo ambayo yana vichaka vya kawaida ndiyo makazi yake makuu utampata.

Kwa watu wengi anasifika kwa kukamata Kuku hasa vifaranga na huenda utakuwa uneshawahi kusikia stori namna anavyokamata kuwa hutumia sehemu ya haja kubwa kama mtego kwa mawindo yake.

Muonekano wa Kicheche mnyama ambae hawezi kuishi bila kujamiiana kabisa!

Jambo hilo halina ukweli, Kwa mujibu wa tafiti zinaonesha namna wanavyofanya ni;

Miguu yao ya nyuma ina nguvu sana tofauti na mbele hivyo hutumia miguu hiyo kukamata baadhi ya wanyama wadogo na kuwabana kwa ustadi mkubwa kitendo ambacho huonekana ni kama ametumia sehemu yake ya haja kubwa kukamata windo.

Ukimuangalia kwa kiasi kikubwa amefanana na Nguchiro’ na huwa na urefu wa sentimita 60 ukijumlisha na mkia wake ambao kwa pekee huwa na urefu hadi sentimita 20.

Muonekano wa meno yake ambayo yanamuwezesha kula Nyama bila shida yoyote

Kwa siku Kicheche’ wana uwezo wa kujamiiana kwa wastani mpaka mara 60 na hiyo ndiyo sababu mojawapo kwa mtu kama anatabia ya kujihusisha kimapenzi na watu wengi kwa mkupuo huitwa Kicheche’ sifa yote imetokea kwa huyu mnyama.

Namna Anavyojihami.

Anapohisi yupo katika hatari mojawapo ya jambo ambalo hufanya ni Kujamba’ ambapo hutoa harufu kali ambayo humtisha adui.

Zaidi kingine ambacho hufanya, Huinua mkia wake na pia mgongo na kuuchanua mfano wa maua ili aonekane mkubwa na kumtisha adui wake.

Kicheche hawa kitaalamu wanaitwa “Striped Polecat”

Chakula chao kikuu ni wanyama wadogo kama Panya, nyoka, chura etc.

SOMA PIA: FAHAMU MAAJABU YA UKUTA WA CHINA (THE GREAT WALL)

Wastani wa maisha yake ni miaka 13 mpaka 15 na kingine Kicheche’ wanapenda kukaa kipekee pekee’ sio wanyama wanaopenda sana ushirikiano. Kwao ushirikiano ni wakati wa kujamiiana tu.

Tuandike lolote hapo chini katika boksi la maoni kuhusu mnyama Kicheche!

Hits: 776